COUTINHO AMVULIA KOFIA INIESTA

Kiungo mshambuaji mpya wa Barcelona, Philippe Coutinho amekiri kuwa Andres Iniesta ana uwezo wa hali ya juu katika kucheza mpira.

Coutinho ambaye alijiunga miamba hiyo ya Hispania akitokea Liverpool mwezi Januari kwa ada ya pauni 142 milioni amesema kiungo huyo ni ‘genius’ wa soka.

Kiungo huyo ameanza mechi mbili akiwa na miamba hiyo amesema anajifunza vitu vingi mazoezini akiwa na Iniesta, Lionel Messi na Luis Suarez.

ÔÇťAndres ni genius sana kila mtu anayecheza pembeni yake atakwambia hili, najisikia furaha kucheza nae pamoja na Leo [Messi], kwangu mimi najifunza vitu kutoka kwako,” alisema Coutinho.

Raia huyo wa Brazil anakutana na upinzani wa namba ndani ya kikosi hicho baada ya kurejea Ousmane Dembele aliyekuwa majeruhi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *