CROATIA YAIFUATA UINGEREZA NUSU FAINALI, WENYEJI URUSI WATUPWA NJE

Croatia imekamilisha idadi ya timu nne zilizofuzu nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuwafunga wenyeji Urusi kwa penati 4-3.

Croatia itakutana na Uingereza siku ya Jumatano katika mchezo wa nusu fainali ya pili baada ya ile ya kwanza ya Ufaransa dhidi ya Ubelgiji.

Mchezo huo ulilazimika kwenda dakika 120 baada ya kumalizika kwa sare ya bao moja katika muda wa kawaida.

Wenyeji Urusi walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 31 kupitia kwa Denis Cheryshev kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Artem Dzyuba.

Croatia walisawazisha bao hilo dakika ya 39 kupitia kwa Andrej Kramaric baada ya kumalizia mpira wa Mario Mandzukic.

Damagoj Vida aliipatia Croatia bao la pili dakika ya 101 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Luca Modric.

Urusi walisawazisha hilo dakika ya 115 ya kupitia kwa Mario Fernandez kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Alan Dzagoev.

Penati za wenyeji zilifungwa na Dzagoev, Ignashevic na Daler Kuzyaev wakati Smolov na Fernandez wakipoteza penati zao.

Penati za Croatia zilifungwa na Marcello Brozovic, Luca Modric, Vida na Ivan Rakitic huku Mateo Kovacic akikosa mkwaju wake.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *