Dakika yoyote Nemanja Matic anatua United

Sky Sports na vyombo vingine vingi vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa uhamisho wa kiungo wa Serbia anayekipiga Chelsea, Nemanja Matic kwenda Manchester United uko katika hatua za mwisho.

Kocha wa United Jose Mourinho amesema anamsubiri Ed Woodwards akamilishe usajili wa wachezaji wawili kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Nemanja Matic akipambana na Marouane Felaini, wawili  hawa wanatazamiwa kucheza pamoja katika safu ya kiungo kama mipango itakaa sawa.

Mtaalam huyo wa mbinu raia wa Ureno aliwahi kusema anahitaji kiungo mmoja na winga mmoja huku hitaji lake la kwanza likiwa ni Perisic ambaye amepeperuka hivyo kumfanya ahamishie majeshi kwa Nemanja licha ya Chelsea kupanga kumuuza Juventus.

Mpinzani wa Matic katika usajili kwenye kikosi hicho cha United alikuwa ni Eric Dier lakini Tottenham Hotspur wameweka wazi kuwa hawapo tayari kumuuza kinda huyo wa Uingereza.

Mourinho aliwahi kufanya kazi na Nemanja katika kikosi cha Chelsea hivyo kuongeza uwezekano wa kiungo huyo kutua United hivi karibuni.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *