Daktari alipeleka taifa changa kabisa kombe la dunia.

TIMU ya taifa ya Iceland hapo jana ilifungua kurasa mpya ya historia kufuatia kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia, baada ya kuichabanga timu ya taifa la Kosovo kwa jumla ya mabao 2 bila majibu.

Iceland inayonolewa na mwalimu ambae anafanya pia kazi ya muda kama daktari wa meno,Heimir Hallgrimsson imefanikiwa kufikisha alama 22 katika msimamo wa kundi lao ikiwa imecheza michezo 10.

Iceland yenye jumla ya watu takriban 350,000 inaingia katika histori ay kua taifa changa kabisa kushiriki kombe la dunia wakivunja rekodi ua Trinidad& Tobago iliyoshiriki kombe la dunia mwaka 2006 wakiwa na jumla ya watu milioni 1.3.

Haya ni mafanikio makubwa kabisa kwa Iceland, inayotamba na aina yao ya kipekee ya ushangiliaji “huuuuh”, ikiongozwa na nyota kama Gylfi Sigurdsson anaekipiga katika kilabu cha Everton nchini England.

Iceland wakishangilia kwa aina yao ya kipeee kabisa “huuuuh”
Iceland iliwahi kuishangaza dunia pia baada ya kuitoa nje England katika mashindano ya mataifa barani ulaya mwaka 2016.

Mataifa mengine yaliyofuzu kushiriki kombe la dunia mpaka sasa ni kama ifuatavyo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *