Daktari anena tatizo linalomtesa Kamusoko.

Kiungo wa kimataifa wa klabu ya Dar es salaam Young Africa maarufu kama Yanga na raia wa Zimbabwe Thabani Kamusoko anaendelea na matibabu chini ya usimamizi wa daktari wa timu hiyo, Nassor Matuzya.

Matuzya ameiambia Simba Makini kwamba Kamusoko anasumbuliwa na kikombe cha goti, jeraha alilolipata katika mchezo dhidi ya Njombe mji na kujitonesha tena katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa jijini Dar es salaam.

Aidha dakatari Matuzya ametaja ubovu wa viwanja vingi vya hapa nchini kua chanzo kikuu cha wachezaji wengi kupata majeruhi na kujitonesha pindi wanappopata nafuu mara kwa mara.

Wachezaji wengine wa Yanga walio majeruhi mpaka sasa ni pamoja na Hamis Tambwe na Donald Ngoma ambao tayari wameshaanza mazoezi mepesi na wanatarajiwa kuwa timamu kabla ya mchezo wao na Kagera Sugar.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *