Daktari awapa somo Yanga

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari wa michezo Tanzania (TASMA), Shecky Mngazija, ameushukia uongozi wa klabu ya Yanga kwa kuunda kamati mbalimbali na kushindwa kuweka ya tiba.

Hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga aliteua wajumbe 55 waliounda jumla ya kamati saba tofauti za kushughulikia masuala mbalimbali ya klabu hiyo.

Clement Sanga

Akizungumza na SIMBA MAKINI jana, Mngazija alisema Yanga wamefanya vizuri kuunda kamati hizo lakini walichokosea ni kitendo cha kushindwa kujumuisha madaktari kwenye mojawapo ya kamati hasa ya ufundi.

“Kama walivyounda kamati nyingine kulikuwa na haja ya kuweka ya tiba itakayoshughulikia afya ya wachezaji kuanzia lishe na pale wanapotaka kusajiliwa, mfano mzuri TFF kuna kamati maalum ya tiba inayojitegemea,” alisema.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *