DE BRUYNE ATAENDELEA KUBAKI MUDA MREFU MAN CITY

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne amesema anatarajia kubaki katika viunga vya Etihad kwa muda mrefu zaidi.

De Bruyne ambaye alijiunga na City akitokea Wolfsburg Agosti 2015 kwa ada ya pauni 54.5 milioni kwa mkataba wa miaka sita alikuwa akifanyiwa mahojiano kuelekea mchezo wao dhidi ya Arsenal mwishoni mwa juma hili.

Tangu alipohamia nchini Uingereza, De Bruyne amekuwa miongoni mwa wachezaji bora akifunga mabao 25 na kusaidia mengine 45 katika michezo 104 ya mashindano yote.

Akiwa na City ambao ndio vinara wa ligi hiyo amesema anapenda maisha ya klabu hiyo chini ya Meneja Pep Guardiola.

Tangu Pep aje kwenye klabu hii, tunacheza staili ya soka ambayo ninaipenda kwahiyo inakuwa rahisi kwangu kufanya vizuri.Napapenda hapa, kuna mazingira mazuri tangu nimejiunga nimekuwa nikiaminiwa sana pia napenda jinsi wanavyo endesha mambo yao, nitaishi kwa muda mrefu,” alisema De Bruyne.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *