DE BRUYNE HAKUPENDA POGBA KUKOSEKANA MANCHESTER DERBY

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City, Kevin De Bruyne hakufurahishwa na kukosekana kwa Paul Pogba katika mchezo wa Manchester derby kwakua anapenda kukutana na wachezaji bora.

Pogba ataanza kutumikia adhabu ya kukosa mechi tatu kufuatia kadi nyekundu alionyeshwa katika mchezo dhidi Arsenal siku ya Jumamosi. Mechi nyingine atakazo kosa ni dhidi ya AFC Bournemouth na West Brom.

“Sipendi kuona mchezaji akipata majeraha, katika mashindano unatakiwa kukutana na timu bora yenye wachezaji bora kama Pogba.

“Katika hili kila mtu ana maoni yake, unaweza kusema chochote ila kwa upande wetu tunajipanga kufanya vizuri katika hali yoyote.

“Pogba ni mchezaji mzuri, simjui sana lakini ni muhimu sana uwanjani. Alipewa kadi nyekundu na atakosa mchezo huu, ni kama amekuwa majeruhi tu kwakua hatoweza kucheza,” alisema De Bruyne.

Miamba hiyo itakutana siku ya Jumapili katika uwanja wa Old Trafford, City ikiwa kinara na pointi 43 wakati United ikiwa ya pili na alama 35.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *