Dejan Lovren asaini mkataba wa muda mrefu Liverpool.

Dejan Lovren, beki wa kimataifa wa Croatia na klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, asubuhi ya leo hii ameingia mkataba wa  muda mrefu wa kuitumikia klabu hiyo katika viunga vya Melwood utakaombakiza klabuni hapo mpaka mwaka 2021 .

Lovren (27) aliejiunga na Liverpool akitokea klabu ya Southampton mwezi julai 2014 mpaka sasa ameshaichezea timu yake mechi 105 na kufanikiwa kufunga magoli 4 sasa atakua akipokea paundi 100,000 kwa juma.

thumb_39697_default_news_size_5thumb_39698_default_news_size_5

Lovren katika viwanja vya Melwood baada ya kusaini mkataba  na klabu yake ya Liverpool.

Beki huyo ametengeneza maelewano mazuri na Joel Matip raia wa Cameroon, wakiisaidia liverpool kuwepo kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya kwa kufungwa mchezo 1  tu kati ya 15 walizocheza pamoja mabeki hao.

Lovren alielezea furaha yake baada ya kusaini mkataba huo kwa kusema ” nafurahishwa na kila kitu hapa klabuni, nataka nibakie hapa na kua sehemu ya familia kwa muda mrefu zaid”

Msimu huu wa 2016/17 Lovren amecheza mechi 28 na kufanikiwa kufunga magoli 2.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *