Dini yamfanya ‘Sheikh’ Lukaku apishane na zawadi Marekani

STRAIKA mpya wa Manchester United Romelu Lukaku alishindwa kuteuliwa kama  mchezaji bora wa mechi (Man Of the Match) katika mchezo dhidi ya Manchester City kutokana na imani ya dini yake ya kiislamu.

Lukaku alionyesha kiwango bora katika mchezo huo uliopigwa jijini Houston Marekani akitupia bao la kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-0 walioupata mashetani hao lakini waandaji walishindwa kumteua kama mchezaji bora kwavile asingeweza kushika zawadi ya kilevi.

Romelu Lukaku

Mashindano hayo yanayofahamika kama International Champions Cup yanafanyika katika uwanja wa NRG na kudhaminiwa na kampuni ya kutengeneza pombe aina ya Heineken.

Klabu zote zilituma majina ya maafisa na wachezaji waislamu pamoja na wale walio chini ya miaka 21 ambao hawaruhusiwi kugusa wala kupiga picha na zawadi za vilevi.

Henrikh Mkhitaryan ambaye alitengenezea bao la pili la United lililofungwa na Marcus Rashford ndiye alipokea zawadi hiyo kama mchezaji bora wa mchezo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *