DISMAS TEN: LWANDAMINA ANARUDI JUMATATU

Baada ya tetesi kuwa kocha George Lwandamina ameikacha Yanga na kujiunga na timu ya Zesco United ya Zambia uongozi wa mabingwa hao umekanusha vikali taarifa hiyo.

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema kocha huyo alienda Zambia baada ya kupata msiba na atarejea siku ya Jumatatu kuendelea na kazi yake.

Vyombo vya habari mbalimbali yakiwemo magazeti yameripoti kuwa Mzambia huyo yuko mbioni kujiunga na Zesco huku mkataba wake na Yanga ukielekea ukingoni.

“Hizo ni taarifa za kwenye mitandao huwezi kuwazuia watu kusema wanachodhani kuwa ni sahihi ila ukweli ni kwamba Lwandamina bado ana mkataba na klabu ya Yanga.

“Alikwenda kwenye matatizo ya msiba kwao Zambia na atarejea siku ya Jumatatu kuandaa kikosi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbeya City,” alisema Ten.

Tetesi zinasema endapo Lwandamina atatimka Boniface Mkwasa ambaye kwa sasa ni katibu mkuu atakiongoza kikosi mpaka mwishoni mwa msimu.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *