DTB MABINGWA WAPYA MICHUANO YA BRAZUCA

Benki ya DTB imeibuka bingwa wa michuano ya mabenki ijulikanayo kama ‘Brazuca’ baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 3-0 dhidi ya Exim katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa kasi kwa timu zote ulilazimika kwenda kwenye hatua hiyo ya penati baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja kwenye muda wa kawaida.

Mabingwa hao wapya walipoteza mchezo wa fainali mwaka jana baada ya kufungwa na NMB katika uwanja huo huo.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na benki ya ABC baada ya kuwachapa Barclay’s.

Mshambuliaji Morison Ngowo wa BancABC aliibuka kinara wa ufungaji wakati Rogers Pembe wa timu hiyo hiyo akiwa bora katika kusaidia ‘Assist’ mabao hayo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *