Emmanuel Martin aipa Yanga ushindi wa jioni

BAO la jioni la Emmanuel Martin limetosha kuipa ushindi wa mabao 3-2 timu ya Yanga dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.

Martin alifunga bao kwenye dakika za nyongeza kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango Said Lubawa na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Yanga waliofurika katika uwanja huo.

Singida walikosa mikwaju miwili ya penati katika mchezo huo dakika ya kwanza na 78 kupitia kwa washambuliaji wake Danny Usengimana na Atupele Green.

Thaban Kamusoko aliipatia Yanga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja nje ya 18 kabla ya Usengimana kuisawazishia Singida kwa kichwa dakika tatu baadae akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Deus Kaseke.

Simba Nhivi aliipatia Singida bao la pili dakika ya 23 kufuatia Canavaro kushindwa kuondoa hatari na kumfanya mfungaji atazamane na kipa Benno Kakolanya kabla hajamchambua.

Singida United wakishangilia bao lao

Kocha wa Yanga George Lwandamina alifanya mabadiliko kwa wachezaji wote kipindi cha pili lakini kasi ya mchezo ilipungua tofauti na kipindi cha kwanza.

Amiss Tambwe aliisawazishia Yanga kwa mkwaju wa penati dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Singida kucheza madhambi ndani ya eneo la hatari.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *