FIRMINO KUIKOSA BOURNEMOUTH

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amethibitisha kuwa mshambuliji wake Roberto Firmino amepata maumivu ya shingo na atakosa mechi ya leo dhidi ya AFC Bournemouth.

Raia huyo wa Brazil alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya katikati ya juma lililopita.

“Bobby amepata maumivu ya shingo lakini anaendelea vizuri nadhani atakuwa poa katika mchezo ujao,” Klopp aliuambia mtandao wa Liverpool.

Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amesema wachezaji Ragnar Klavan na Nathaniel Clyne nao wana hati hati ya kukosa mchezo huo kutokana na majeraha.

Firmino amekuwa mchezaji muhimu wa Liverpool msimu huu baada ya kufunga mabao 23 katika mashindano yote.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *