FRED KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA MAN UNITED LEO

kiungo wa Skakhtah Donetsk, Fred atafanyiwa vipimo vya afya leo ili kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Manchester United kwa mujibu wa Sky Sports.

Nyota huyo alicheza dakika 82 katika ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Brazil jana dhidi ya Croatia uliopigwa katika uwanja wa Anfield ambapo utakuwa usajili wa kwanza wa Meneja Jose Mourinho majira haya ya joto.

Sky Sports inafahamu kuwa tangu mwezi Mei United ilikuwa kwenye mazungumzo mazuri na Fred ambaye mwezi Januari alihusishwa na Manchester City.

Fred 25, alijiunga na Shakhtar kutoka Internacional ya Brazil mwaka 2013 na tayari ameichezea miamba hiyo ya Ukraine zaidi ya mechi 150.

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Tite amesema hajashangazwa na United kumuhitaji Fred lakini ametaka dili hilo likamilike haraka ili aendelee kuandaa kikosi chake kwa kombe la dunia.

“Kama ikitokea itakuwa haizuiliki atakuja kwetu kuomba ushauri na jambo hili nashauri limalizike mapema ili arejeshe mazingatio kwenye timu ya Taifa,” alisema Tite.

Brazil itacheza mechi nyingine ya kirafiki Juni 10 dhidi ya Austria katika mji wa Vienna kabla ya kuelekea moja kwa moja Urusi wakiwa kundi E pamoja na timu za Switzerland, Costa Rica na Serbia.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *