Ghana yamkatia rufaa mwamuzi wa mchezo dhidi ya Uganda.

Ghana imepeleka malalamiko yake katika shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kufuatia sare ya mchezo wao dhidi ya Uganda uliowafutia kabisa matumaini ya kufuzu kombe la dunia nchini Urusi.

Ghana maarufu kama “The Black stars” waliekea katika mchezo huo uliopigwa jijini kampala wakihitaji zaidi ushindi kuendelea kuweka matumaini ya kufuzu kwenye kundi E, waliishia kuduwazwa baada ya goli la halali kabisa walilofunga katika dakika za nyongeza kukataliwa na mwamuzi.

Chama cha mpira nchini Ghana (GFA) kimesema, malalamiko hayo dhidi ya maamuzi mabovu ya mwamuzi kutona nchini Afrika ya kusini Daniel Bennet pamoja na wasaidizi wake Eldrick Adelaide na Steve Marie wote kutokea Seychelles yalipelekwa mara tu mpira huo ulipomalizika.

GFA imeiomba FIFA kufikiria kuurudia mchezo huo ili haki iweze kupatikana.

Bofya hapa kutazama goli linalolalamikiwa na Ghana..

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *