GOR MAHIA YAPATA TIKETI YA KWENDA GOODISON PARK

Mabingwa wa Kenya timu ya Gor Mahia imefanikiwa kupata tiketi ya kwenda uwanja wa Goodison Park kucheza na Everton baada ya kuifunga Simba mabao 2-0 katika mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Gor kucheza na Everton kwani mwaka jana pia walikutana katika uwanja wa taifa Dar es Salaam baada ya kuibuka mabingwa.

Gor imemaliza michuano ikiwa haijaruhusu nyavu zake kuguswa hata mara moja huku wakifunga mabao saba.

Mshambuliaji Maddie Kagere aliifungia Gor bao la mapema dakika ya sita baada ya kupokea safi ya Jacques Tuyisenge.

Kagere ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara pili mfululizo baada ya kufunga mabao manne.

Tuisenge aliifungia Gor bao la pili kwa dakika ya 55 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo Humphrey Mieno.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *