Gor Mahia yawatangulia Everton Dar

TIMU ya Gor Mahia kutoka Kenya imewasili nchini mchana wa leo tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Everton kutoka Uingereza utakaofanyika keshokutwa katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Gor ndio mabingwa wa michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika hapa jijini Dar es Salaam mwezi uliopita na kushirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya zinazodhaminiwa na Kampuni hiyo ya michezo ya bahati nasibu.

Everton pia inadhaminiwa na Kampuni hiyo huku ikitarajiwa kutua na kikosi chake kamili chini ya kocha Ronald Koeman akiwemo mshambuliaji Wayne Rooney aliyesajiliwa wikiendi iliyopita akitokea Manchester United.

Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr (kushoto) atakiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza tangu ajiunge nacho juma lililopita

Timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza itatumia mchezo huo kama maandalizi ya kabla ya kuanza ligi kuu Agosti 12.

Kiingilio cha chini kwenye mchezo kitakuwa shilingi 3,000 kwa mzunguko huku kikubwa kikiwa shilingi 8,000 huku mchezo huo ukitarajiwa kuanza saa 11 jioni.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *