Guardiola, Harry kane,Antonio Valencia wang’aa tuzo za mwezi Septemba.

KOCHA mkuu wa klabu ya Manchester City, Pepp Guardiola ameibuka kinara mbele ya makocha wote wa ligi kuu nchini Uingereza kwa mwezi septemba akichagizwa na ushindi alioupta dhidi ya Liverpool,Chelsea,Crystal Palace na Watford.

Guardiola ameanza vizuri msimu huu akishinda mechi 6 kati ya 7 walizocheza mpaka sasa huku safu zake za ulinzi, kiungo pamoja na ushabuliaji zikionekana kuimarika vyema tofauti na msimu uliopita.

Guardiola na wasaidizi wake katika picha ya pamoja.

Tuzo nyingine ilikwenda kwa Harry Kane, akitunukiwa uchezaji bora wa mwezi septemba baada ya kuifungia klabu yake ya Tottenham mabao 6 katika mechi 4 za mwezi wa septemba zikiwemo goli 2 katika mchezo dhidi ya Westham. Hivi majuzi Harry Kane akiwa nahodha alifanikiwa pia kufunga bao muhimu lilioipeleka England kombe la dunia nchini Uruusi mwaka 2018.

Harry Kane akionyesha tuzo yake ya mwezi septemba.

Tuzo nyingine imekwenda kwa mlinzi wa Manchester United, Antonio Valencia akipewa tuzo ya goli bora kufuatia mkwaju wa nguvu maarafu kama “Volley” katika mchezo dhidi ya Everton.

Antonio Valencia akionyesha tuzo yake leo hii.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *