GUARDIOLA: MAN UNITED INAWEZA KUTWAA TAJI LA EPL

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola amewaonya wachezaji wake kuwa majirani zao Manchester United wanaweza kutwaa taji la ligi kuu Uingereza kama wao wasipojipanga vizuri.

Wiki iloyopita United ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya City na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye uwanja wa Etihad.

“Hisia zangu ni kwamba United watavuna pointi nyingi kwakua wapo kwenye kiwango bora na wana wachezaji wazuri, wanaweza kushinda mechi zote sita zilizobaki.

Novemba na Disemba mwaka jana tulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa lakini ndani ya wiki moja tumepoteza mechi tatu.

“Tunahitaji kushinda mechi zetu, lakini tupo kwenye presha kubwa kwa sasa, kama itatokea tutashindwa kutwaa taji msimu huu tutawapa hongera kubwa United,” alisema Guardiola.

City itasafiri hadi jijini London leo kuifuta Tottenham Hotspur katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Wembley.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *