Gyan sasa mambo fresh, ‘atatesti’ mitambo na Azam

MSHAMBULIAJI mpya wa timu ya Simba raia wa Ghana, Nicholas Gyan atawasili nchini Jumamosi asubuhi kujiunga na Wekundu hao baada ya kumaliza mkataba wake na waajiri wake wazamani.

Gyan 19, amesajiliwa na Simba akitokea Ebusua Dwarfs FC inayoshiriki ligi kuu nchini Ghana ambayo iligoma kumuachia hadi amalize mkataba wake kabisa.

Kupitia katika ukurusa wake wa Instagram msemaji wa Wekundu hao Haji Manara ameandika kuwa mchezaji huyo atawasili nchini Septemba 2 baada ya mkataba wake kumalizika.

“Mshambulaji wetu Nicholas Gyan atawasili nchini Septemba 2 na kocha Joseph Omog akiona inafaa atamtumia katika mchezo dhidi ya Azam FC Septemba 6,” alisema Manara.

Gyan (kulia) akiwa na Niyonzima mara baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari

Gyan amekosa mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting pamoja na ule wa ngao ya jamii waliowafunga watani wao Yanga kwa penati 5-4 katikati ya wiki iliyopita.

Ujio wa mshambuliaji huyo kijana utampa kocha Omog wigo mpana zaidi wa kuchagua kikosi kufuatia uwepo wa nyota kama Emmanuel Okwi, John Bocco, Laudit Mavugo na Juma Liuzio.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *