HAKUNA WAKUIZUIA MAN CITY, ARSENAL YAPIGWA TATU ETIHAD

Kasi ya timu ya Manchester City iliyoanza nayo tangu kuanza msimu huu bado haijapata dawa baada ya kuifunga Arsenal mabao 3-1 katika mchezo wa ligi ya Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa Etihad.

Tangu kuanza kwa msimu City imekuwa ikitoa vipigo vikubwa huku ikiwa bado haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Vijana hao wa kocha Pep Guardiola walimiliki sehemu kubwa ya mchezo huo ambapo mara kadhaa mlinda mlango Peter Cech wa Arsenal alikuwa kwenye wakati mgumu.

Mabao ya City yalifungwa na Kelvin De Bruyne, Sergio Aguero na Gabriel Jesus wakati lile la Arsenal likifungwa na Alexander Lacazzate.

City imefikisha pointi 31 ikiendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo baada ya mechi 11.

Katika mchezo wa awali Tottenham Hotspur iliifunga Crystal Palace bao moja katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *