HANSPOPE: KAPOMBE KAMA HUTAKI KUCHEZA ‘SEPA’

Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi beki wa kulia Shomari Kapombe ameambiwa na uongozi wa Simba kuwa anaweza kuondoka kama hatacheza.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hanspope akisema kuwa kiraka huyo tayari amepona majeraha yake lakini hataki kucheza.

Hanspope amesema inaonekana beki huyo anaogopa kugombania namba kutokana na usajili mkubwa uliofanyika kikosini msimu huu.

“Hatuwezi kuwa tunamlipa mchezaji anayekaa benchi kila siku wakati tunafahamu kuwa amepona.

“Ninamwambia kuwa achague kama anataka kucheza ili aendelee kubaki Simba kama hawezi aondoke, hatuwezi kumlipa mtu halafu hatumtumii,” alisema Hanspope.

Pamoja na uwezo kipaji kikubwa alichopewa Kapombe lakini majeruhi ya mara kwa mara yamekuwa yakimkwamisha.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *