Hatupaki basi, Liverpool jiandaeni kuzuia washambulaji 9 – Mourinho

Nitacheza na mlinzi mmoja na washambuliaji tisa

ni maneno ya Jose Mourinho alipoulizwa kuhusu aina yake ya mchezo mara nyingi anapocheza na timu kubwa.

Manchester itaingia katika dimba la Anfiled hapo kesho kupambana na wapinzani wao wa jadi liverpool,mchezo utaokchezwa mapema majira ya saa 8 kwa saa za Afrika mashariki. Manchester inaingia katika mchezo huo ikiwa imeshinda michezo 6 kati ya 7 bila ya kupoteza hata mchezo mmoja na kujikusanyia alama 19 huku wapinzani wao wakiwa wameshinda michezo 3, kwenda sare 3 na kufungwa mchezo 1.

Bofya hapa kumsikiliza Jose Mourinho.

Wakati Mourinho akijinadi, Kocha wa Liverpool Jurgen Klop amewaambia mashabiki wa liverpool kwamba yeye ni bora zaidi kwa sasa na wasifikiirie kumtimua ingawa timu imekua haipati matokeo mazuri kwa sasa

Kama watanifukuza kwa sasa,siamini kama kuna walimu wengi wazuri wanaoweza kuifanya kazi hii zaid yangu mimi

Klopp ameendelea kwa kusema kikosi cha Liverpool kimeimarika zaid tangu alipoanza kukinoa misimu miwili iliyopita.

Liverpool itamkosa kiungo wake muhimu Sadio Mane ambae taarifa za daktari zimesema atakaa nje kwa takribani majuma 6 huku ikiwa na matumaini ya mchango mkubwa kutoka kwa Andre Coutinho ambaye alianza msimu akiwa na majeruhi.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *