Hawa Manchester City Mtawakoma Kwenye Usajili

KLABU ya Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola imepata bajeti kubwa kwa ajili ya usajili wa majira ya joto ili kuboresha kikosi hicho kwa msimu wa 2017/18

Klabu hiyo ina bajeti ya paundi 250 milioni ambayo wamejiandaa kusajili majembe kama Alexis Sanchez, Benjamin Mendy, Kyle Walker, Ryan Bertrand, Virgil Van Dijk pamoja na kinda wa Anderlecht Youri Tielemans ili kuifanya timu hiyo kutisha katika kila idara.

Kufuatia klabu hiyo kutolewa katika hatua ya robo fainali klabu bingwa barani Ulaya na kupata wakati mgumu kwenye vita ya kugombania ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza huenda Guardiola akasajili wachezaji hao ili apate matokeo anayoyahitaji.

Sanchez-711679

City imeshindwa kutisha msimu huu kama ambavyo wengi walitarajia hasa baada ya ujio wa mtaalamu Guardiola na sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu baada ya kushuka dimbani mara 33 na kujikusanyia pointi 65.

Kama Guardiola ataweza kuchanga vema karata zake kwenye matumizi ya pesa hizo kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikatisha zaidi msimu ujao tofauti na huu unaomalizika.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *