HAZARD ASEMA ATASAINI MKATABA MPYA CHELSEA

Kiungo mshambuliji Eden Hazard amethibitisha kuwa hataondoka Chelsea ambapo yeye na mlinda mlango Thibaut Courtois watasaini mikataba mipya na mabingwa hao.

Hazard 27, alikuwa miongoni wa wacheza soka waliohudhuria mchezo wa kikapu kati ya Boston Celtics dhidi ya Philadelphia katika uwanja wa O2 Arena jijini London ambapo alisema hataondoka.

Chelsea inafanya jitihada za kuhakikisha inamshawishi nyota huyo kuongeza mkataba mpya ambao unamalizika mwaka 2020.

Mwezi uliopita baba mzazi wa nyota huyo Thierry Hazard alisema mtoto wake hataongeza mkataba na matajiri hao wa London ili kupata nafasi ya kujiunga na Real Madrid.

Courtois pia alionyesha dhamira ya kutaka kuondoka na kujiunga na Madrid baada ya mkataba wake kumalizika Juni 2019 lakini anaonekana kubadili maamuzi na kuendelea kusalia klabuni hapo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *