HIMID: TUTATUMIA UZOEFU KUIA ZANZIBAR LEO

Nahodha wa timu ya Tanzania bara ‘Kili Stars’ Himid Mao amesema watatumia uzoefu walionao kuibuka na ushindi dhidi ya ndugu zao Zanzibar Heroes katika mchezo wa utakaofanyika leo kwenye uwanja wa Kenyatta.

Mchezo huo wa kundi A ni muendelezo wa michuano ya Cecafa Chalenji inayo endelea nchini Kenya inayoshirikisha timu tisa.

Himid alikosekana kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya uliomalizika kwa sare ya bila kufungana amesema anaamini aina ya wachezaji waliopo kikosini wanaweza kuwafanya kutoka na alama zote tatu.

Kiungo huyo Azam FC amesema kurejea kwake kikosini kutaongeza nguvu katika mchezo huo huku akiahidi ushindi.

“Tutatumia uzoefu kuhakikisha tunashinda mchezo wa leo ingawa mechi itakuwa ngumu kwakua Zanzibar sio timu mbaya ila sisi tumewazidi,” alisema Himid.

Kili Stars itakosa huduma ya mshambuliaji Mbaraka Yusuph aliyepata maumivu kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Libya.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *