HIZI HAPA SABABU ZA ZANZIBAR, ETHIOPIA KUENGULIWA MASHINDANO YA U17

Timu za Taifa chini ya miaka 17 za vijana za Zanzibar ‘Karume Boys’ na Ethiopia zimetolewa katika michuano ya vijana inayoendelea nchini Burundi kutokana na wachezaji wake kuzidi umri.

Wachezaji wa timu hizo walifanyiwa vipimo vya MRI jana na kugundulika wamezidi umri hivyo wamekosa vigezo vya kuendelea na mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Burundi zinasema baada ya vipimo wachezaji nane wa Zanzibar ndio walikuwa na vigezo vya kucheza michuano hiyo huku wengine wakizidi umri.

Timu hizo zilipaswa kupeleka wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 lakini wao wamepeleka wenye miaka 17 hivyo wamevunja kanuni za mashindano.

Zanzibar na Ethiopia zimepigwa faini ya dola 15000 kila mmoja na kufungiwa kutoshiriki mashindano hayo kwa mwaka mmoja.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *