HUU HAPA USAJILI WA KWANZA WA DAVID MOYES, WEST HAM

Meneja mpya wa West Ham David Moyes amemtaja mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings kuwa usajili wake wa kwanza mwezi January.

Moyes aliyechukua nafasi ya Slaven Bilic aliyefutwa kazi wiki chake zilizopita anataka kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkopo wa muda mrefu.

Ings amekosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jurgen Kloop kitu ambacho kinaweza kumfanya mshambuliaji huyo kukubali mara moja ofa hiyo.

Mbali na West Ham mshambuliaji huyo mwenye miaka 25, pia anatakiwa na klabu za Newcastle na Bournemouth zinazoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Moyes amekuwa shabiki mkubwa wa Ings ambapo alihitaji saini yake tangu akiwa wa kocha wa Real Sociedad ya Hispania.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *