ITALIA ISIPO KAZA HAIENDI URUSI MWAKANI

Italia ipo kwenye hati hati ya kutoshiriki michuano ya kombe la dunia mwakani nchini Urusi kufuatia kupata kipigo cha bao moja kutoka kwa Sweden katika mchezo wa kwanza wa mtoano.

Mabingwa hao wa dunia mwaka 2006 imewalazimu kucheza mechi ya mtoano baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye hatua ya makundi.

Mchezo wa marudiano utafanyika nchini Italia siku tatu zijazo ili kupatikana mshindi wa jumla ambaye atapata tiketi ya kwenda Urusi mwakani.

Senegal imefuata nyayo za Misri na Nigeria baada ya kufuzu fainali hizo kwa kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0 kwenye uwanja wa Peter Mokaba.

Matokeo ya awali ya mchezo huo uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana yalifutwa baada kutokea kwa kashfa ya upangaji wa matokeo na mwamuzi wa mchezo huo Joseph Lamptey kutoka Ghana alifungiwa maisha kujihusisha na soka.

Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utafanyika siku ya Jumanne jijini Dakar, Senegal ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba.

Matokeo ya mechi za kufuzu zilizopigwa

Sweden 1-0 Italia

Honduras 0-0 Australia

Algeria 1-1 Nigeria

South Africa 0-2 Senegal

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *