KAGERA YASHINDA, YAPANDA NAFASI MBILI

Timu ya Kagera Sugar imepata ushindi wa bao moja nyumbani mbele ya Mwadui FC na kupanda nafasi mbili kwenye msimamo wa ligi.

Kagera ilikuwa nafasi ya 14 na pointi zake 18 ambapo ushindi umeisogeza hadi nafasi ya 12 ikifikisha alama 21.

Tangu kuanza kwa msimu Kagera inayonolewa na kocha Mecky Mexime imekuwa ikipata matokeo mabovu na kujikuta ikiendelea kubaki chini katika msimamo.

Licha ya kushindwa kupata matokeo katika michezo mingi lakini Wana Nkulukumbi hao wamekuwa wakionyesha soka safi huku safu yao ya ushambuliaji ikikosa umakini.

Katika mchezo huo bao la Kagera lilifungwa na Japhet Makarai kipindi cha kwanza na kuwafanya kujikwamua kutoka chini.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *