KAKAMEGA KUTOWAFIKISHA SINGIDA KWENYE PENATI

Timu ya Kakamega Homeboyz imejipanaga kupata matokeo katika muda wa kawaida dhidi ya Singida United katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya SportPesa Super Cup.

Katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba juzi walitolewa kwa mikwaju ya penati 5-4 kitu ambacho hawataki kitokee tena kesho katika mechi dhidi ya Singida.

Nahodha wa timu hiyo, Estone Esiye amekiri kuwa Singida ni timu nzuri na wanatagemea kupata upinzani mkubwa lakini watahakikishia wanapata ushindi katika muda wa kawaida.

Esiye amesema wataingia kwa kushambulia kwa kasi katika mchezo huo ili kupata ushindi katika muda wa kawaida.

“Katika michezo wa kesho tutaingia kwa kushambulia zaidi kuliko ilivyokuwa mechi ya Simba tunahitaji kushinda kabla ya kufika hatua ya penati,” alisema Esiye.

Mchezo huo utaanza saa 7 alasiri ukifuatiwa na mechi ya fainali kati ya Simba dhidi ya Gor Mahia.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *