Kane, Ronaldo uso kwa uso wembley wakiwa vinara wa mabao.

Nyota wa Totenham Harry Kane pamoja na Christiano Ronaldo wa Real Madrid wanangoza kwa idadi ya magoli ya kufunga mpaka sasa wakiwa wamepachika jumla ya mabao 5 katika mechi 3 walizocheza kwenye kombe la mabingwa barani ulaya. Totenham watajitupa uwanjani kucheza na Real Madrid katika dimba la Wembley siku ya kesho wakichagizwa na sare ya bao 1 kwa 1 kwenye mchezo wao uliopita katika uwanja Santiago Bernabéu.

Wanaofuatia kwa idadi ya mabao mpaka sasa ni kama ifuatavyo,

Wissam Ben Yedder 3 (Sevilla)
Edinson Cavani 3 (PSG)
Dimitri Oberlin 3 (Basel)
Vincent Aboubakar 2 (Porto)
Mohamed Salah 3 (Liverpool)
Roberto Firmino 3 (Liverpool)
Cenk Tosun 3 (Beşiktaş)
Edin Džeko 3 (Roma)
Lionel Messi 3 (Barcelona)
Romelu Lukaku 3 (Man. United)
Neymar Jr. 3 (PSG).

Michezo ya ligi ya mabingwa barani ulaya inatazamiwa kuendelea tena leo na kesho kukamilisha mzunguko wa nne. Simba Makini itakuletea “Link” itakayokuwezesha kutazama mechi zote mubashara kupitia kipakato chako au simu yako ya kiganjani.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *