Kapombe aachwa Stars inayokwenda Rwanda

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kitaondoka nchini kesho mchana kuelekea Kigali, Rwanda kikitokea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa marudioni wa michuano ya (CHAN) dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ bila ya beki Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi.

Kapombe aliumia katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba na kumalizika kwa sare ya bao moja ambapo beki huyo alitolewa dakika ya 20 hivyo hataweza kusafiri na timu hiyo.

Stars ipo jijini Mwanza kwa kambi kabla ya mchezo huo ambapo itapitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere kwenda Rwanda.

Kapombe akipelekwa vyumbani wakati wa mapumziko

Kikosi hicho kitaondoka jijini humo kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania saa nne asubuhi na kitawasili Dar es Salaam saa sita mchana kabla ya kuunganisha na ndege ya Rwanda saa nane mchana kwenda Kigali.

Stars inapaswa kuibuka na ushindi katika mchezo huo au kupata sare ya kuanzia mabao mawili na zaidi ili kufuzu hatua inayofuata.

Mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Uganda na Sudan Kusini ambazo zilitoka sare katika mchezo wao wa kwanza, mechi za mwisho kabla ya kufuzu zitachezwa baadae mwezi ujao.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *