Kauli ya baba wa kinda anayetisha kwa ‘kutupia’ Ujerumani

BERLIN, Ujerumani
BABA kinda wa miaka 12 Youssoufa Moukoko aliyefunga mabao matatu katika timu ya vijana ya Ujerumani chini ya miaka 16 amewatoa hofu watu wanaotilia shaka umri wake.

Moukoko amefunga bao dhidi ya Austria Jumatatu na kufunga mengine mawili katika mchezo wa marudiano uliofanyika Jumatano ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Youssoufa Moukoko

Tayari kinda huyo amefunga mabao 13 katika klabu yake ya Borussia Dortmund kwenye kikosi cha vijana chini ya miaka 17.

“Baada ya kuzaliwa, tulimuandikisha katika ubalozi wa Ujerumani jijini Yaounde, tuna cheti cha kuzaliwa kutoka Ujerumani” alisema mzazi huyo ajulikanae kwa jina la Joseph.

Kwa mujibu wa cheti halisi cha kuzaliwa , Moukok alizaliwa Novemba 20,2004 nchini Cameroon.

Kumekuwa na maswali mengi kutoka katika vyombo vya habari nchini Ujerumani kuhusu umri halisi wa kinda huyo lakini chama cha soka nchini humo (DFB) kimekiri kuwa umri wake ni sahihi.

Kwa mujibu wa sheria za DFB, Moukoko hatoruhusiwa kucheza ligi kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ hadi afikishe miaka 17.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *