Khune “fiti” langoni mwa Bafana Bafana kuwavaa Senegal usiku huu.

Golikipa wa Bafana Bafana, Itumeleng Khune ametajwa kwenye kikosi kitakachoanza dhidi ya Senegal usiku wa leo katika kuwania kufuzu michuano ya fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwakani.

Kulikua na hatihati ya mlinda mlango huyo kuwepo leo kufuatia maumivu ya uso aliyoyapata katika mchezo wa ligi kuu nchini Afrika ya kusini mwishoni mwa juma hili.

kikosi kamili kitakachoanza leo hii ni Itumeleng Khune, Clayton Daniels, Morgan Gould, Thamsanqa Mkhize, Sifiso Hlanti, Dean Furman, Kamohelo Mokotjo, Lebogang Manyama, Themba Zwane, Sibusiso Vilakazi, Percy Tau.

Wachezaji wa akiba, Wayne Sandilands, Ronwen Williams, Motjeka Madisha, Tebogo Langerman, Eric Mathoho, Siphiwe Tshabalala, Phakamani Mahlambi, Tiyani Mabunda, Keagan Dolly, Bradley Grobler.

kikosi hicho kitaongozwa na mwalimu Stuart Baxter, katika mchezo ambao Afrika ya kusini lazima washinde ili kuweka matumaini ya kufuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *