KICHUYA AIPAISHA SIMBA MBEYA, YAREJEA KILELENI

Bao pekee lililofungwa na winga Shiza Kichuya limetosha kuipa ushindi Simba na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kuifunga Mbeya City katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sokoine.

Kichuya alifunga bao hilo mapema dakika ya saba baada ya kupokea pasi ndefu iliyopigwa kutoka katikati ya uwanja na kiungo Jonas Mkude.

Simba imefikisha pointi 19 sawa na Azam FC lakini kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga Wekundu hao wanarejea kileleni.

Baada ya bao hilo Simba iliendelea kuliandama lango City huku wakimiliki sehemu kubwa ya mchezo mpaka wanaenda mapumziko.

Kipindi cha pili City walirudi kwa kasi wakati Simba wakionekana kuwa taratibu hali iliyo sababisha kocha Joseph Omog kumtoa kiungo Haruna Niyonzima na kumuingiza Said Ndemla dakika ya 56 ili kuongeza nguvu.

Mabadiliko hayo yaliifanya safu ya kiungo ya Simba kutulia na kupunguza kasi ya wachezaji City na matokeo kubaki kama yalivyokuwa.

Baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa wikiendi ijayo Simba itashuka katika uwanja huo huo kucheza na Tanzania Prisons.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *