KIIZA HASHIKIKI, AIPAISHA SIMBA

NA MWANDISHI WETU

kiizaaa

MSHAMBULIAJI Hamis Kiiza ‘Diego’ wa Simba leo jioni ameibuka shujaa katika uwanja Taifa jijini Dar es Salaam, baada ya kuifungia mabao matatu timu yake katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Kiiza alifunga mabao hayo kati8ka ushindi wa mabao 3-1, huku mabao hayo yakipatikana katika dakika za 30, 46 na la mwisho akifunga sekunde chache kabla  ya dakika za nyongeza kumalizika.

Kutokana na mabao hayo Kiiza amefikisha idadi ya mabao  matano katika mechi tatu za ligi kuu alizocheza ambapo idadi hiyo haijafikiwa na mchezaji yoyote hadi sasa

Bao pekee la Kagera Sugar liliwekwa kimiani na mshambuliaji wao Mbaraka Yusuph, baada ya walinzi wa Simba kushinda kuondoa mpira eneo la hatari dakika ya 56.

Hii imekuwa ni faraja kwa mashabiki wa Simba baada ya msimu uliopita kucheza mechi sita mfululizo bila kushinda hata mchezo mmoja.

Simba ilianzia mechi zake zote za msimu huu wa ligi kuu bara, mkoani  Tanga  na kujikusanyia pointi  sita ambako ilicheza mchezo kwa kwanza dhidi ya African Sport na kushinda bao 1-0, mechi ya pili walicheza na Mgambo JKT na kutoka na ushindi wa mabao 2-0.

Kutokana na ushindi Simba imejikusanyia pointi tisa huku ikikabiliwa na kibarua kigumu watakapokutana na watani wao wa jadi Yanga mwishoni mwa wiki hii.

Kwa upande wa Kagera Sugar inayonolewa na kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita, Mbwana Makatta  unakuwa ni mchezo wa pili kupoteza. Kagera walipoteza dhidi ya Mbeya City  pamoja na Majimaji.

Kikosi cha Simba: Peter Manyika ,Emery Nibomana, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Justice Majabvi, Ibrahim Ajib/ Mwinyi Kazimoto, Simon Sserunkuma, Said Ndemla, Hamis Kiiza na Peter  Mwalyanzi,

Kikosi Cha Kagera Sugar, Agathony Anthony, Salum Kanoni,  Said Hassan, Ibrahim Job, Deogratius Julius, George Kavilla, Iddy Kurachi, Laurence Mugia, Mbaraka Yusuph, Daud Jumanne na Paul  Ngalyoma.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *