KILIMANJARO STARS VYUMA VIMEKAZA CECAFA CHALENJI

Timu ya taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) imetoka sare ya bila kufungana na Libya katika michuano ya Cecafa Chalenji inayo endelea nchini Kenya.

Mchezo huo wa pili wa kundi A umefanyika katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos ikishuhudiwa timu hizo kumaliza mchezo bila kuona nyavu.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja huo huo wenyeji Kenya waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’.

Libya ilicheza vizuri kipindi cha kwanza kwa kushambulia na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini safu ya ulinzi ya Kili Stars ilikuwa imara na mlinda mlango Aishi Manula alionyesha umahiri mkubwa.

Kipindi cha pili Kili ilicheza vizuri ikitengeneza nafasi kupitia kushoto ambapo mlinzi Gadiel Michael alipiga krosi kadhaa ambazo hazikutumiwa vizuri.

Michuano hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili ilitakayopigwa katika kituo cha Kakamega.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *