Kim Poulsen ataja kikosi 50 wa Ngorongoro Heroes

KOCHA mkuu wa Timu za vijana za Taifa Kim Poulsen ametaja kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ambacho kitakuwa kwenye maandalizi kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za Afrika AFCON (U20).

“Nimechagua vijana 50 lakini zaidi ni wale walioshiriki michuano ya AFCON (U17) nchini Gabon wakiwa na kikosi cha Serengeti Boys kutokana na uzoefu walionao, vipaji pamoja na kujituma kwao,” alisema Poulsen.

Wachezaji aliowataja kutokea Serengeti ni Ramadhani Kabwili, Samwel Brazio, Kelvin Kayego, Kibwana Shomari, Asadi Juma, Kevin Naftari, Issa Makamba , Nickson kilobage, Ibrahim Abdallah na Yohana Mkomola.

Wengine ni Nickson Kilomage, Enrick Vitalis, Mohamed Rashid, Patrick Mwenda, Shabani Ada, Cyprian Mutesigwa, Abdul Suleiman, Hamis SuleimaN, Ally Husseni na Marima Makame.

Wachezaji wengine ambao wamepatikana katika michuano mbali mbali ya U20 na wengine katika mashindano ya UMISETA ni Ramadhan Kawambwa, Hassan Kapela, Najm Mussa, Rashid Chambo, Maziku Amani, Hamisi Mustafa, Daruwesh Shariboko, Joseph Lukas, Abdul Twalib Msheti, Samson Peter na Saidi Mohammed.

Wengine ni Ayubu Mohammed, Vitalis Mayanga, Rajabu Adas, Mohamed Mussa, Rifat Hamisi, Rashid Juma, Ramadhan Mohamed, John Kwiyemba, Ramadhan Ramadhan, Oscar Masai, Maulid Lembe, Ibrahim Hueni na Asumani Maulid.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *