KINGUE FITI KUWAVAA NJOMBE MJI, AJUMUISHWA KIKOSINI

Kiungo Mcameroon wa Steven Kingue ni miongoni mwa wachezaji 22 wa Azam FC watakao safari kesho kuelekea mkoani Njombe kwa ajili ya mchezo dhidi ya Njombe Mji siku ya Jumamosi.

Kiungo huyo wa ulinzi alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na maumivu ya mguu lakini baada ya kupona amejuimuishwa kwenye kikosi kwa ajili mchezo huo.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema kikosi cha timu hiyo kitaondoka kesho alfajiri kwa usafiri wa basi kuelekea Njombe tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi.

Jaffer amesema watamkosa kiungo wao Bryson Raphael kwenye mchezo huo baada ya kupata majeraha.
“Kesho alfajiri tutasafiri kuelekea mkoani Njombe kwa ajili ya mechi siku ya Jumamosi, kikubwa ni kurejea kwa kiungo wetu Steven Kingue lakini tutamkosa Bryson,” alisema Jaffer.

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *