KIPIGO CHA KCCA CHAMKIMBIZA KOCHA WA AL AHLY

Taarifa kutoka klabu ya Al Ahly inasema kocha wao mkuu Hossam Al Badry amejiuzulu baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa KCCA katika mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika.

Mabao ya Saddam Juma na Timothy Awany yalitosha kuwapa ushindi miamba hiyo ya Uganda mbele ya mabingwa hao wenye rekodi kubwa Afrika.

Kupitia mtandao wa Twitter klabu hiyo imethibitisha kukubali barua ya kujiuzulu kwa kocha Hossam kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya jana dhidi ya KCCA.

“Kamati ya utendaji imekubali kocha Hossam Al-Badry kujiuzulu,” ulisomeka ujumbe huo kwenye mtandao wa Tweeter.

Timu hiyo kutoka Misri ilitoka sare ya bila kufungana na Esperance ya Tunisia katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Cairo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *