KIPIGO CHA ZENJI CHAIWEKA PABAYA KILI STARS CHALENJI

Timu ya Kilimanjaro Stars imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zanzibar Heroes na kujiweka kwenye nafasi mbaya ya kufuzu hatua inayofuata katika michuano ya Cecafa Chalenji inayofanyika nchini Kenya.

Stars ipo mkiani mwa kundi A ikiwa na alama moja pekee kufuatia sare ya bila kufungana iliyopata dhidi ya Libya katika mchezo wa kwanza.

Katika mchezo huo Stars ilizidiwa sehemu kubwa ambapo ilikuwa haikutengeneza nafasi yoyote mpaka dakika ya 28 Himid Mao alipofunga hilo bao la kufuatia machozi.

Vijana wa kocha Hemed Morocco walicheza kwa maelewano makubwa na walifanikiwa kusawazisha dakika ya 66 kupitia kwa Kassim Khamis.

Ibrahim Ahmada ndiye aliyepeleka kilio kwa Kili Stars baada ya kufunga bao la pili dakika ya 78 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kassim Selembe.

Zanzibar ndio vinara wa kundi A wakiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi zote mbili za hatua ya makundi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *