KIUNGO WA SOUTHAMPTON AMVULIA KOFIA GUARDIOLA

Kiungo wa Southampton, Pierre-Emile Hojbjerg amesema kuwa hakuna Meneja bora kwa sasa Ulimwenguni anayemzidi Pep Guardiola wa Manchester City.

Hojbjerg alikuwa chini ya Guardiola kwa misimu mitatu wakiwa Bayern Munich lakini hii leo watakuwa wapinzani wakati Southampton wakisafiri kuwafuata City katika mchezo wa ligi ya Uingereza.

Guardiola ameiongoza City kushinda michezo 12 kati 13 tangua kuanza kwa ligi msimu huu ambapo Hojbjerg hashangazwi na mafanikio ya Mhispania huyo.

“Jamaa ni kocha wa tofauti sana, hakuna zaidi yake kwa sasa, anafundisha soka kwa staili ya kuvutia inayo muwezesha kutwaa mataji.

“Kila mtu anapenda kutazama, kila anayefanya kazi nae analijua hili anajituma sana katika kutimiza majukumu yake.

“Kila siku, kila muda anatafuta mbinu mpya za kushinda mechi. Ni mtu anayependa kushinda mataji muda wote, kwangu mimi ni mmoja wa makocha bora wa soka niliowahi kuwaona,” alisema Hojbjerg.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *