Kiwanja cha Yanga charejeshwa serikalini

MIEZI kadhaa iliyopita kampuni ya Yanga Yetu Ltd iliyosajiliwa rasmi kwa dhumuni la kuendesha klabu ya Yanga kwa mtindo wa ‘mkodisho’ iliikabidhi klabu hiyo eneo lenye ukubwa wa hekari 715 huko Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na kituo cha michezo.

Mchakato huo ulikuwa kimya kwa kipindi kirefu hasa baada ya kukwama kwa zoezi la kuikodisha klabu kwa kampuni hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu.

Leo hii kupitia ukurasa rasmi wa Facebook wa redio ya Clouds FM imetoka taarifa kuwa Rais John Magufuli amefuta umiliki wa shamba hilo pamoja na jingine la Amadol lenye ukubwa wa hekari 5,400 na kuyarudisha serikalini.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *