KIYOMBO WA MBAO ATISHA TUZO ZA VPL, MWEZI DISEMBA

Mshambuliaji aliye kwenye kiwango bora kwa sasa kutoka timu ya Mbao FC, Habibu Kiyombo amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara mwezi Disemba.

Katika mwezi huo kulichezwa mechi moja ya mzunguko wa 12 wa ligi ambapo nyota huyo alicheza vizuri zaidi ya wengine.

Mshambuliji huyo anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya ufungaji wa ligi kuu akifikisha mabao saba bao moja nyuma ya Emmanuel Okwi wa Simba.

Kiyombo alifunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-0 uliopita Mbao dhidi ya Yanga katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Disemba 29.

Kiyombo atapewa pesa taslimu sh milioni moja na wadhamini wakuu wa ligi kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, ngao pamoja na kisambuzi cha Azam TV kama zawadi baada ya kushinda tuzo hiyo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *