Kocha mpya Barca aanza na ushindi El Classico

MIAMI, Marekani
KOCHA mpya wa Barcelona Ernesto Valverde ameanza kwa ‘zali’ El Classico yake ya kwanza kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid usiku wa kuamkia leo nchini Marekani.

Mchezo huo wa kirafiki ni maandalizi ya msimu mpya wa ligi inayotarajiwa kuanza mwezi ujao ambapo miamba hiyo ya Hispania ipo Marekani ikicheza mechi kadhaa za kujipima ubavu kabla ya kurejea nchini Hispania.

Valverde amechukua mikoba ya kocha Jose Enrique lakini bado wadau wengi wa soka hawampi nafasi kubwa ya kufanya vizuri licha ya kuibuka na ushindi katika michezo yote mitatu ya kirafiki ya maandalizi. Barcelona iliifunga 2-0 Juventus, ikaifunga pia Manchester United bao kabla jana kuwafunga mahasimu hao.

Kovacic kulia akimtoka Andres Iniesta

Mbele ya mashabiki 66,014 katika uwanja Hard Rock, Barca walipata mabao mawili ya haraka kupitia kwa Lionel Messi (3) na Ivan Rakitic (6) kabla ya Mateo Kovacic na Marco Ansensio kusawazisha kabla ya timu hizo kwenda mapumziko.

Beki Gerrard Pique aliifungia Barcelona bao la ushindi dakika ya 50 na kumfanya kocha huyo kuwa na mwelekeo mzuri kabla ya kuanza kwa ligi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *