KOTEI ASHANGAA KUZUSHIWA ANAONDOKA SIMBA

Kiungo wa timu ya Simba, James Kotei amesikitishwa na taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anataka kutimka kwa mabingwa hao.

Jana kulitoka taarifa kuwa kiungo huyo anatimka ili kuungana na mkewe nchini Ghana ambaye anafanya kazi Serikalini.

Kotei ameiambia Simba Makini kuwa taarifa hizo sio za kweli zimetungwa ili kumuharibia na kumgombanisha na waajiri wake Simba.

“Mkataba wangu na Simba unaisha mwaka 2019, bado naipenda Simba na sijafikiria kuondoka kwa sasa,” alisema Kotei.

Kotei ni miongoni mwa wachezaji 20 wa Simba waliosajiliwa kushiriki michuano ya kombe la Kagame inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mghana huyo anatarajiwa kuwepo katika kikosi cha Simba kitakachocheza na JKU ya Zanzibar katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kagame.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *