KUWAONA SIMBA VS YANGA , SHARTI UWE NA BUKU SABA

NA MWANDISHI WETU
SIMBAYANGA
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limeweka wazi viingilio vya mchezo wa ‘Watani wa Jadi’ Simba na Yanga, katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, utakaochezwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa.
Viingilio hivyo vimetangazwa leo mchana kwenye Ofisi za Shirikisho hilo jijini humo ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Sh. Elfu saba (7,000).
Taarifa iliyotumwa na Ofisa Habari wa shirikisho hilo Baraka Kizuguto, ilisema kuwa kiingilio cha juu kitakuwa Sh. ilingi Elfu Thelathini
(30,000) kwa viti vya VIP A, 
 
Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C, 
 
huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000) kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa Ijumaa kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni – Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry – Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya daladala.
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia tiketi ili kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.
“Kumekuwa na sintofahamu nyingi juu ya uzwaji wa tiketi ambako mara nyingi kuna baadhi ya mashabiki wanakuja milangoni wakiwa na tiketi bandia, hivyon ni vyema kila shabiki kwenda sehemu maalum kwa ajili ya kujipatia tiketi yake halali na sio kununua sehemu nyingine ambayo hatujaitangaza” ilimaliza taarifa ya Kizuguto.
It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *