LIGI DARAJA LA KWANZA KUSIMAMA KUPISHA DIRISHA LA USAJILI

Raundi ya tisa ya michuano ya ligi daraja la kwanza itakamilika mwishoni mwa kwa timu zote shiriki kushuka dimbani kabla ya kusimama kwa muda.

Baada ya kukamilika kwa raundi hiyo ligi hiyo itasimama kwa mwezi mmoja kupisha dirisha la usajili kabla ya kuendelea tena kumalizia mechi zilizobaki.

Ofisa Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amewakumbusha waamuzi kuchezesha kwa kufuata sheria ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wadau wa mchezo huo unaopendwa zaidi duniani.

“Waamuzi tumewapa dhamana kubwa wanachotakiwa kufanya ni kuchezesha kwa haki na kufuata sheria 17 za soka.

“Baada ya kukamilika zoezi la usajili ligi itaendelea kwa raundi tano zilizobaki ili kupata timu sita zitakazo panda daraja msimu ujao,” alisema Wambura.

Ligi hiyo imekuwa na msisimko mkubwa msimu huu huku katika makundi yote matatu yakitakiwa kutoa timu mbili kwakua msimu ujao wa ligi utashirikisha timu 20.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *